Waziri mkuu kassimu Majaliwa |
Kibaha.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa amewataka wananchi kila
mmoja kuwa mlinzi wa amani kwa kujilinda na kuwalinda jirani ili kukabiliana na
matukio ya uvamizi na uhalifu ambayo yameanza kujitokeza maeneo mbalimbali
nchini.
Majaliwa amesema kumeibuka matukio ya uvamizi, hivyo lazima
kila mmoja ayatambue mambo yote hatarishi na awe mlinzi ili kukabiliana
nayo.
Kauli hiyo ameitoa tayari yakiwa yametokea matukio makubwa
mawili ya kushambuliwa na kujeruhiwa kwa risasi Mbunge wa Singida Mashariki,
Tundu Lissu ambaye anaendelea na matibabu jijini Nairobi, Kenya na Meja Jenerali
mstaafu Vincent Mritaba.
Amesema hayo leo Jumanne alipozungumza na viongozi wa
Serikali, vyama vya siasa ngazi ya wilaya na mkoa na wafanyakazi wa kiwanda
cha sabuni cha Keds kilichopo Kibaha, akiwa ziarani kutembelea viwanda
mjini hapa.
"Ni hatari kama jambo hili la uvamizi litaendelea hadi
kwa wawekezaji kwa sababu hatuna uhakika hawa wanaoendesha matukio haya nia yao
ni nini kwa Taifa hili, hivyo kila mtu awe mlizi. Naomba mkoa muwalinde hawa
wawekezaji," amesema.
Amesema Serikali imejipanga vyema kudhibiti hali hiyo, hivyo
ameomba wananchi waiunge mkono katika kupambana na watu ambao wanaendelea
kupoteza na kuathiri maisha ya wengine.
Hii ni mara ya nne ndani ya mwaka huu kwa waziri mkuu
kufanya ziara mkoani Pwani kukagua shughuli za uwekezaji wa viwanda.
@habari toka mwananchi
No comments:
Post a Comment