Tuesday, 19 September 2017

Watumishi wa vituo vya afya wilaya ya Nsimbo wametakiwa kufanya kazi zao kwa weledi ili kuweza kutoa huduma bora kwa wananchi


NSIMBO
Watumishi wa vituo vya afya  Halmashauri ya wilaya ya Nsimbo mkoani katavi wametakiwa kufanya kazi zao kwa weledi ili kuweza kutoa huduma bora kwa wananchi wanaowazunguka.
Wito huo umetolewa na diwani wa kata ya katumba Seneta Baraka wakati wa mkutano uliofanyika katika zahanati ya kaminula uliohusisha viongozi wa kijiji ,madiwani wa viti maalumu, pamoja na wauguzi wa zahanati hiyo kwa lengo la kuyapatia ufumbuzi  malalamiko ya wananchi dhidi ya wauguzi wa  zahanati hiyo.


Aidha amewataka wahudumu wa zahanati hiyo kufanya kazi kwa ushirikiano na wananchi ili kuondoa migongano ambayo inakwamisha maendeleo kwa ujumla na kuleta malalamiko kwa wagonjwa.


Hata hivyo mkutano huo umefanyika baada ya kupata malalamiko kutoka kwa wananchi juu ya lugha chafu na wahudumu pamoja na vitendo ambavyo wanafanyiwa wakati wanakwenda kupatiwa huduma.

No comments:

Featured post

MASIKINI WEEE!!!!! KICHANGA CHA SIKU MOJA CHAOKOTWA KATIKA KIWANJA CHA MPIRA AZIMIO

Na;Ezelina Yuda Mtoto mchanga mwenye jinsia ya Kike anayekadiriwa kuwa wa siku 1 ameokotwa akiwa hai kandokando ya uwanja wa azimio  ...