MPANDA
Zaidi ya mwezi mmoja sasa walio kuwa wakazi wa kitongoji cha
Mgolokani kata ya Starike halmashauri ya Nsimbo mkoani Katavi wanaishi chini ya miti.
Aliyekuwa Mwenyekiti
wa kitongoji cha mgolokani Bw.Divason Kisulo ambaye amesema tangu operesheni ifanyike ya kuondoa
wananchi katika maeneo hayo kwa madai kuwa ni hifadhi ya misitu hakuna sehemu
mbadala iliyotengwa kwaajili ya makazi mapya.
Kwa upande wake mwenyekiti wa halmashauri ya Nsimbo Bw. Raphael
Kalinga Amesema hilo ni suala la
kisheria na kuwataka wananchi kuwa na subira wakati mamlaka husika zikilifanyia
kazi.
Zoezi la kuwaondoa
wananchi katika maeneo mbali mbali yanayo daiwa kuwa ni sehemu ya hifadhi za
misitu limefanywa katika wilaya zote mkoani Katavi .
No comments:
Post a Comment