MPANDA.
Baadhi ya
wakazi wa Kijiji cha Manga kilichopo
Manispaa ya Mpanda wameulaumu uongozi wa serikali ya kijiji hicho
kushindwa kuwadhibiti wafugaji wanaojihusisha na uharibifu wa mazingira.
Wakizungumza
na Mpanda radio fm mapema leo wamesema kuwa kwa kiasi kikubwa uchomaji wa
misitu katika eneo hilo unafanywa na wafugaji lakini hawaoni hatua zozote
zikichukuliwa.
Kwa upande
wa Mwenyekiti wa kitongoji cha Manga Bw,Jackson Kapisula amekili kuwepo kwa
uharifu huo na kuitaja sababu kuwa ni kukithiri kwa ufugaji holela.
Kijiji cha
Manga kipo kata ya Kasokola kaskazini mwa mkoa wa Katavi ambapo ndio kitovu cha
maji ya mserereko maarufu kama Ikolongo yanayotumika katika Manispaa ya Mpanda.
No comments:
Post a Comment