Saturday, 14 October 2017

Mkuu wa wilaya ya Tanganyika amewataka wananchi wanaoishi Kalumbi katika kijiji cha Mpembe, Lyamgoloka katika eneo la ushoroba,Igalukilo,Bariadi, na Misanga Wilayani humo kuondoka haraka katika maeneo hayo.



TANGANYIKA.
Mkuu wa wilaya ya Tanganyika Salehe Muhando amewataka wananchi wanaoishi  Kalumbi katika kijiji cha Mpembe, Lyamgoloka katika eneo la ushoroba,Igalukilo,Bariadi, na Misanga Wilayani humo  kuondoka haraka katika maeneo hayo. 

Ametoa Tamko hilo leo wakati akizungumza na Mpanda Redio  na kusema kuwa  tayari muda uliokuwa umetolewa umekwisha.                                        
Muhando amesema wananchi wa  Bariadi, Igalukilo na Misanga wanatakiwa kurudi katika maeneo ya Luhafwe yaliyotengwa kwa ajili ya makazi yao, huku Wananchi wa kalumbi wanatakiwa kurudi katika eneo la makazi la kijiji cha Mpembe. 
Amesema kuwa kumekuwa na matukio ya uvamizi wilayani humo mengine yakihusishwa na silaha za moto jambo ambalo hutokana na watu kukaa katika maeneo yasiokuwa na Mamlaka kamili za utawala na hivyo wahalifu  kugeuza maeneo hayo kama sehemu ya kujiicha.
Aidha Ameongeza kuwa kumekua na taarifa za kurejea wananchi walioondolewa katika eneo la  Lyamgoloka  na kuwataka  kuondoka haraka kabla ya hatua kuchukuliwa.
@habari na Mdaki Hussein

No comments:

Featured post

MASIKINI WEEE!!!!! KICHANGA CHA SIKU MOJA CHAOKOTWA KATIKA KIWANJA CHA MPIRA AZIMIO

Na;Ezelina Yuda Mtoto mchanga mwenye jinsia ya Kike anayekadiriwa kuwa wa siku 1 ameokotwa akiwa hai kandokando ya uwanja wa azimio  ...