MPANDA
JUMLA ya wanafunzi 14 katika
Halmashauri ya Wilaya ya Nsimbo Mkoani Katavi,wamepata ujauzito katika kipindi
cha mwezi Januari hadi juni mwaka huu.
Takwimu hiyo imetolewa na Afisa
ustawi wa jamii wa halmashauri hiyo Dianarose Mnuo wakati akizungumza na Mpanda
Radio kuhusu namna wanavyodhibiti mimba za utotoni na utoaji elimu kwa jamii.
Kati ya wanafunzi hao 14,wanafunzi
watano wanatoka shule ya msingi za Ugalla,Katumba na Kanoge huku 9 wakitoka Shule
za sekondari Katumba,Nsimbo na Sitalike.
Hata hivyo leo mkoa wa Katavi unafanya
kongamano ili kujadili matatizo ya mtoto wa kike ikiwa ni kuelekea kilele cha maadhimisho ya
siku kike Duniani yanayoadhimishwa Oktoba 11 ya kila mwaka.
Kitaifa mwaka huu yanaadhimishwa Mkoani
Mara ambapo Kaulimbiyu inasema’’Siku ya kimataifa ya mtoto wa
kike,tokomeza mimba za utotoni tufikie uchumi wa viwanda’’
@Habari na Rebeka Kija.
No comments:
Post a Comment