Mkuu wa wilaya ya Tanganyika Salehe Muhando |
TANGANYIKA.
Mkuu
wa wilaya ya Tanganyika mkoa wa Katavi
Salehe Muhando amesema kamati ya ulinzi na usalama itaendelea kutumia
nguvu katika
zoezi
la kuwaondoa wananchi katika maeneo ambayo siyo makazi.
Ametoa
kauli hiyo kwa njia ya Simu, na
kufafanua kuwa tukio la kufariki kwa mtu mmoja katika kitongoji cha Mnyamasi
kata ya Tongwe wakati maafisa misitu wakitekeleza zoezi hilo kimetokana na wananchi kutotii sheria.
Aidha
ameongeza kusema kuwa zoezi hilo ni endelevu na kuwataka wananchi watii sheria
bila shuruti.
Mpaka
sasa imeripotiwa kuwa zaidi ya watu saba wamejeruhiwa tangu kuzuka kwa vurugu
hizo mnamo oct 7/2017.
@habari na Mdaki Hussein
No comments:
Post a Comment