Tuesday, 10 October 2017

Mstahiki Meya wa manispaa ya Mpanda William Mbogo amezindua mradi wa maji ya bure unao fadhiriwa na kampuni la GBP mkoani Katavi


KATAVI.
Mstahiki Meya wa manispaa ya Mpanda William Mbogo  amezindua mradi wa maji ya bure unao fadhiriwa na kampuni la  GBP linalojihusisha na uuzaji wa mafuta ya Petrol.

Akizungumza katika uzinduzi uliofanyika katika kituo cha GBP kilichopo kata ya Majengo mjini Mpanda amewataka wakazi wa eneo hilo kuutumia mradi huo vizuri ili udumu zaidi.
  
Kwa upande wa Meneja wa Kampuni la GBP katika kituo hicho amesema kampuni hilo limeamua kutoa huduma ya maji kutokana na kuona adha ya maji inavyo wakabili wakazi wa eneo hilo.


Miongoni wa wananchi walio jitokeza katika hafla hiyo wamesema  mradi huo ni ukombozi kwa akina mama na familia kwa ujumla.
  

Mradi huo unatoa zaidi ya lita lakimoja kwa siku ambapo utawanufaisha wakazi wa kata ya majengo na maeneo jirani.

No comments:

Featured post

MASIKINI WEEE!!!!! KICHANGA CHA SIKU MOJA CHAOKOTWA KATIKA KIWANJA CHA MPIRA AZIMIO

Na;Ezelina Yuda Mtoto mchanga mwenye jinsia ya Kike anayekadiriwa kuwa wa siku 1 ameokotwa akiwa hai kandokando ya uwanja wa azimio  ...