TANGANYIKA.
Mkuu wa wilaya ya Tanganyika Salehe Muhando ameviagiza vyombo vya
ulinzi na usalama kupita na kuwasaka watu wanaojihusisa na matukio ya mauji ya
watu wilayani humo ili kukomesha vitendo
hivyo.
Muhando ametoa agizo hilo wakati akizungumza na Mpanda Redio baada
ya kuripotiwa matukio ya watu kuuawa kwa kukatwa mapanga huku mengine
yakihusisha silaha za moto wilayani humo.
Amesema hawataruhusu kikundi au watu waendelee kutamba, kutishia
au kuhatarisha usalama na amani kwa kupoteza maisha ya watu na kuwataka wanaomiliki silaya wajisalimishe.
Aidha amewataka watendaji katika ngazi za vijiji kutowaruhusu watu
kuingia katika maeneo yao bila kutambulika huku akiwahakikishia wananchi wa
wilaya ya Tanganyika Kuvidhibiti vitendo hivyo kwa kipindi cha muda mfupi.
No comments:
Post a Comment