DAR ES
SALAAM
Serikali
imetakiwa kuchukua hatua juu ya uharibifu wa mazingira unaoendelea katika Ziwa
Rukwa, vinginevyo madhara zaidi yataendelea.
Wito huo umetolewa na wataalamu wa mazingira waliokutana jijini
Dar es Salaam kuzungumzia sheria kinzani ambazo zinasababisha hatari za
mazingira.
Ambwene Yona kutoka Shirika lisilo la Serikali linalojishughulisha
na utunzaji mazingira Mkoa wa Rukwa (Ramso), alisema Ziwa Rukwa lina uwezo wa
kulisha wanyama 43,800 lakini mpaka sasa limevamiwa na mifugo 167,900 jambo
ambalo ni hatari.
Eden Wayimba kutoka Shirika la Uhifadhi wa Mazingira (Kaeso), amesema
migogoro iliyokuwapo Rukwa imesababishwa na wafugaji.
@habari na Mwananchi
No comments:
Post a Comment