Mkutano mkubwa unaounga mkono uhuru wa Catalonia kutoka Hispania unatarajiwa kufanyika mjini Barcelona leo, wakati mgogoro wa kisiasa nchini humo ukiendelea.
Kiongozi wa zamani wa Catalonia Carles Puigdemont na mawaziri wengine wanne wa zamani ambao wako uhamishoni Brussels, wanatarajiwa kufikishwa mahakamani nchini Belgium, na kuweza kurudishwa tena Hispania.
Awali Puigdemont aliwataka viongozi wa Muungano wa Ulaya kutoa hakikisho kwamba wataunga mkono matokeo ya uchaguzi wa jimbo hilo mwezi ujao hata kama uchaguzi huo utasababisha jimbo hilo kujitenga na Hispania.
Katika hotuba yake kwa Mameya wa Catalonia ambao watakwenda Brussels, ameuliza kama viongozi hao wataendelea kuunga mkono kile alichokitaja kuwa mapinduzi ya kijeshi yaliyofanywa na waziri mkuu wa Hispania Maria Rajoy.
Chanzo: Bbc swahili
No comments:
Post a Comment