Thursday, 9 November 2017

Waziri mkuu wa Tanzania Kasimu Majaliwa amesema vyombo vya ulinzi na usalama vinauwezo wa kukabiliana na vitendo vyote vya uhalifu.

Waziri mkuu wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Kasimu Majaliwa 


DODOMA

Waziri mkuu wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Kasimu Majaliwa amesema vyombo vya ulinzi na usalama vinauwezo wa kukabiliana na vitendo vyote vya  uhalifu.

Amesema hayo wakati akijibu swali la Kambi rasmi ya Upinzani lililoulizwa na mkuu wa Kambi hiyo Freeman Mbowe aliyetaka kujua dhamira ya serikali kuchunguza tukio la kushambuliwa kwa risasi kwa mbunge wa Singida Mashariki Tundu Lissu (CHADEMA).

Katika majibu yake ya msingi waziri mkuu amesema vyombo vya dola nchini vinafanya uchunguzi wa tukio hilo na kuwataka watanzania kuwa na imani na vyombo vyao vya ulinzi na usalama.

Aidha amefafanua kuwa uchunguzi wa matukio ya namna hiyo huwa yanafanywa na watu kwa kutumia mbinu nyingi hivyo hata uchunguzi wake huwa unafanyika kwa utaratibu na uangalifu mkubwa  

Source Haruna Juma




No comments:

Featured post

MASIKINI WEEE!!!!! KICHANGA CHA SIKU MOJA CHAOKOTWA KATIKA KIWANJA CHA MPIRA AZIMIO

Na;Ezelina Yuda Mtoto mchanga mwenye jinsia ya Kike anayekadiriwa kuwa wa siku 1 ameokotwa akiwa hai kandokando ya uwanja wa azimio  ...