MPANDA
JAMII
Mkoani Katavi imeaswa kushirikiana ipasavyo na kamati ya kulea baraza la watoto
wenye ulemavu iliyopo Wilayani Mpanda Mkoani Katavi kwa kuwafichua watoto
waliofichwa majumbani ili wapatiwe haki ya elimu.
Wito
huo umetolewa jana na Meneja wa Mradi wa elimu jumuishi Tanzania Alani Kamunde
wa shirika la International Aid Service,kupitia kikao cha
kupokea,kujadili,kutathimini na kupanga mikakati ya namna ya kuyapatia ufumbuzi
matatizo yanayowakabili watoto wenye ulemavu Mkoani Katavi.
Kwa
upande wake mratibu wa mradi wa elimu Jumuishi mikoa ya Rukwa na Katavi
Bi.Veronica Mavanza amesema,matatizo yanayowakabili watoto wenye ulemavu
yaliyobainishwa na kamati ya kulea
baraza la watoto wenye ulemavu wameyachukua na watashirikisha jamii
ipasavyo kuyapatia ufumbuzi.
Nao
baadhi ya wajumbe wa kamati hiyo inayolea watoto wenye ulemavu wamesema uwepo
wa mradi wa elimu Jumuishi Mkoani Katavi umesaidia jamii kutambua haki za
watoto wenye ulemavu ikiwemo kuwapeleka shule na kuwapatia haki nyingine muhimu
za kibinadamu.
Mradi
wa elimu Jumuishi uliopo katika mikoa ya Rukwa na Katavi pekee hapa
nchini,unaratibiwa na shirika la IFI lenye makao makuu Mkoani Arusha
likijumuisha washirika watatu ICD,IAS na kanisa la FPCT
Source ISSACK GERALD
No comments:
Post a Comment