ZANZIBAR
Wanawake nchini wametakiwa kuwa tayari katika kufanya kazi pamoja na kuzitumia ipasavyo fursa mbalimbali za kujiendeleza kimaisha ili kwenda sawa na malengo ya serikali ya kukuza uchumi na kupunguza umaskini.
Mratibu wa Kampeni ya kuhamasisha wanawake na kutoa elimu ya kutengeneza bidhaa mbalimbali za ujasiriamali Abla Mohammed Baraka amesema wanawake wamekuwa wakichangia pato la taifa hivyo ni vyema kusimama imara katika kujiunga na vikundi vya ushirika ili kujikimu na kuondokana na utegemezi.
Amesema utegemezi wa wanawake katika familia unachangia kwa kiasi kikubwa kufanyiwa vitendo vya udhalilishaji hivyo ni vyema kujiamini katika kufanya shughuli za maendeleo ili kujikwamua na hali ngumu ya maisha.
Kampeni ya kuhamasisha wanawake ijulikanayo kwa jina la wanawake chakarika imekuwa ikitoa elimu mbalimbali kwa wajasiriamali ili wapate ujuzi zaidi ikiwemo utengenezaji wa Sabuni za aina tofauti na utafutaji wa masoko.
Source-Zanzibar24,Editor:Issack Gerald
No comments:
Post a Comment