Tuesday, 14 November 2017

MRADI wa skimu ya umwagiliaji ya Ng'ongo wilayani Sumbawanga unazidi kupungua uwezo wakuzalisha mazao siku hadi siku kutokana na ukosefu wa maji.




RUKWA

MRADI wa skimu ya umwagiliaji ya Ng'ongo wilayani Sumbawanga mkoani Rukwa unazidi kupungua uwezo wakuzalisha mazao siku hadi siku kutokana na ukosefu wa maji pamoja na wafugaji wanaofuchungia mifugo katika eneo hilo.

Akizungungumza mbele ya mkuu wa mkoa wa Rukwa mwenyekiti wa mradi wa scheme ya umwagiliaji ya Ng'ongo Justine Amon alisema kuwa kwa kipindi cha mwaka 2015/2016 wakulima waliweza kulima hekta 128 nakufanikiwa kuzalisha tani 460.8 za mahindi.

Amesema kuwa katika msimu wa mwaka 2016/2017 katika hekta hizo 128 uzalidhaji umeshuka hadi kufikia tani 358.4 kutokana na sababu mbalimbali ikiwemo haribifu wa mazingira pamoja na wafugaji kuchungia ndani ya eneo la uzalishaji. 

Kwaupande wake mkuu wa mkoa wa Rukwa Joachim Wangabo alisema kuwa iliuzalishaji uweze kuongezeka ni lazima sheria ndogo za halmashauri zitumike kuwabana waharibifu wa mazingira. 

 

No comments:

Featured post

MASIKINI WEEE!!!!! KICHANGA CHA SIKU MOJA CHAOKOTWA KATIKA KIWANJA CHA MPIRA AZIMIO

Na;Ezelina Yuda Mtoto mchanga mwenye jinsia ya Kike anayekadiriwa kuwa wa siku 1 ameokotwa akiwa hai kandokando ya uwanja wa azimio  ...