DODOMA
Serikali imesema tozo inayotozwa na jeshi la zima moto
na uokoaji kwa lengo la kutoa kibali cha ujenzi ni kwa mujibu wa sheria ya
mwaka 2015.
Hayo yamesemwa na Naibu
waziri wa wizara ya mambo ya ndani ya nchi Mhandisi Hamad Masauni
wakati akijibu swali mbunge wa jimbo la mpanda mjini Sebastiani Kapufi
alilotaka kujua kama tozo hizo zipo kihalali ili wananchi waweze kuendelea
kutozwa
Aidha naibu waziri
amesema ili kuondokana na majanga yanayotokana na ujenzi holela lazima wananchi
walipie tozo hiyo ili wapate kibali cha ujenzi.
Jeshi la zima moto na
uokoaji mkoa wa katavi wiki iliyopita ilitangaza kushuka kwa bei ya tozo hiyo
kutoka shilingi laki moja na nusu na kufikia elfu hamsini ili kila mwananchi
aweze kuimudu.
Source
Tbc
No comments:
Post a Comment