KAGERA
Diwani
wa Kata ya Buhangaza wilayani Muleba Samsoni Makoti (49) amefariki dunia jana
Jumapili jioni katika Hospitali ya Kagondo wakati akipatiwa matibabu baada ya
kuugua kwa muda mrefu.
Mwenyekiti
wa Halmashauri ya Wilaya ya Muleba, Chrizant Kamugisha amesema mwili wa diwani
huyo utahifadhiwa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Kagera kusubiria taratibu za
mazishi
Kamugisha
amesema madiwani wote 57 wa halmashauri hiyo watakutana leo Jumatatu kwa ajili
ya kuunda kamati ya mazishi na baadaye kuufuata mwili ili uweze kuagwa na
wana Muleba.
Amesema
kwa muda mrefu diwani huyo alisumbuliwa na kisukari na baadaye kupooza upande
mmoja wa mwili hivyo amepelekwa katika hospitali mbalimbali kuokoa maisha yake
lakini haikuwezekana.
Source 24
Editor Safina Joel
No comments:
Post a Comment