DAR
ES SALAAM
Mahakama Kuu ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
imemhukumu kwenda jela miaka miwili muigizaji wa filamu bongo
Elizabeth Michael (Lulu) ambaye alikuwa anakabiliwa na kesi ya kuua bila
kukusudia.
Hukumu hiyo imetolewa leo na Jaji Sam Rumanyika aliyekuwa
anaendesha kesi hiyo, na kusema kwamba mshtakiwa amekutwa na hatia ya kuua bila
kukusudia kutokana na ushahidi wa mazingira, hivyo atatumikia kifungo cha miaka
miwili jela.
Baada ya hapo Jaji Rumanyika aliwapa nafasi upande wa
mshtakiwa kujitetea ambapo wakili wake Peter Kibatala alimtetea mshakiwa kwa
kusema kuwa mshtakiwa anategemewa na familia yake akiwemo mama yake na mama
yake mdogo.
Aidha Jaji Rumanyika alitoa hukumu yake na kumuamuru
mshtakiwa kwenda jela kwa miaka miwili.
Elizabeth Michael (Lulu) anahukumiwa kwa kumuaa aliyekuwa
mpenzi wake Steven Charles Kanumba ambaye pia alikuwa ni muigizaji mwenzake,
mnamo April 7, 2012.
No comments:
Post a Comment