Tuesday, 21 November 2017

Serikali ya Mapinduzi Zanzibar inampango mkubwa wa kuimarisha ulinzi kwa kuweka vifaa vya kisasa katika maeneo ya bandari na viwanja vya ndege ili kuweza kupunguza mambo mabli mbali ambayo nihatarishi nchini.



 Mh Aboud Mohammed



ZANZIBAR

Serikali ya Mapinduzi Zanzibar inampango mkubwa wa kuimarisha ulinzi kwa kuweka vifaa vya kisasa katika maeneo ya bandari na viwanja vya ndege ili kuweza kupunguza mambo mabli mbali ambayo nihatarishi nchini.

Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais Mh Aboud Mohd amesema Serekali imezingatia umuhimu wa kuimarisha ulinzi katika maeneo hayo kwa kuweka vifaa vya kisasa ilikupambana na wimbi la uhalifu likiwemo usafiarishaji  wa madawa ya kulevya.

Aidha Aboud amesema Ofisi yake inawahamasisha  na kuwapatia elimu wananchi ya kuepukana na matumizi ya madawa ya kulevya ambayo ni hatarishi kwa vijana na taifa hapo baadae.

Kwa upande wake kamanda wa Polisi Mohd Salum Mohd ameishukuru kamati hiyo kwa kutembelea  bandarini hapo na kusema kuwa changamoto nyingine ni kuwepo kwa bandari bubu ambazo zinatumiwa na wahalifu hao.


SOURCES:MWANANCHI

No comments:

Featured post

MASIKINI WEEE!!!!! KICHANGA CHA SIKU MOJA CHAOKOTWA KATIKA KIWANJA CHA MPIRA AZIMIO

Na;Ezelina Yuda Mtoto mchanga mwenye jinsia ya Kike anayekadiriwa kuwa wa siku 1 ameokotwa akiwa hai kandokando ya uwanja wa azimio  ...