Mkuu wa Mkoa wa Geita, Robert Gabriel ameiagiza Halmashauri ya Geita kufanya ukaguzi ili kujua kama fedha ambazo Kata ya Mgusu inapewa na Mgodi wa Dhahabu Geita (GGM), zinatumika kwa malengo yaliyokusudiwa.
Mgodi wa Dhahabu Geita (GGM)
GEITA
Mkuu wa Mkoa wa Geita, Robert
Gabriel ameiagiza Halmashauri ya Geita kufanya ukaguzi ili kujua kama fedha
ambazo Kata ya Mgusu inapewa na Mgodi wa Dhahabu Geita (GGM), zinatumika kwa
malengo yaliyokusudiwa.
Agizo hilo amelitoa baada ya
kupokea malalamiko ya wananchi wa Mtaa wa Mgusu waliodai kuwa GGM hutoa fedha
kila mwezi kutokana na kazi zinazofanywa na vijana wa mtaa huo ndani ya mgodi,
lakini hawajui mapato na matumizi ya fedha hizo.
Diwani wa kata hiyo, Pastory
Ruhusa amesema hakuna shule ya sekondari jambo ambalo hulazimu wanafunzi
kutembea zaidi ya kilomita 20 kwenda shule za kata nyingine.
Afisa uhusiano wa jamii wa GGM, Manase Ndoroma
amesema mgodi huo umekuwa ukichukua vijana kwenye mitaa na vijiji
vinavyouzunguka ambao hulipwa Sh300,000, na kati ya fedha hizo Sh60,000 hurudi
kwenye ofisi za vijiji kwa shughuli za maendeleo.
No comments:
Post a Comment