Tuesday, 21 November 2017

Serikali imesema itaendesha msako na kuvifunga vyuo vyote vya afya visivyokidhi vigezo na msharti ya uwepo wake.


Naibu Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dk. Faustine Ndugulile


 

DAR ES SALAAM

Serikali imesema itaendesha msako na kuvifunga vyuo vyote vya afya visivyokidhi vigezo na msharti ya uwepo wake.

Hayo yamesemwa jijini Dar es Salaam na Naibu Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dk. Faustine Ndugulile, wakati akizungumza  kwenye mahafali ya Chuo cha Tiba na Afya cha KAM.

Amesema ingawa ni kweli kuna uhaba mkubwa wa watumishi wa sekta ya afya, lakini serikali haiwezi kuvumilia vyuo ambavyo vinajiendesha bila kufuata miongozo ya serikali.

Aidha, waziri huyo alisema serikali inatambua na kuthamini mchango mkubwa unaotolewa na vyuo binafsi hivyo itaendelea kushirikiana navyo kutatua changamoto mbalimbali ili viweze kustawi na kutoa wahitimu wengi zaidi watakaosaidia taifa.

SOURCE:mwananchi

No comments:

Featured post

MASIKINI WEEE!!!!! KICHANGA CHA SIKU MOJA CHAOKOTWA KATIKA KIWANJA CHA MPIRA AZIMIO

Na;Ezelina Yuda Mtoto mchanga mwenye jinsia ya Kike anayekadiriwa kuwa wa siku 1 ameokotwa akiwa hai kandokando ya uwanja wa azimio  ...