Aliyekuwa makamu wa rais wa Zimbabwe Emmerson
Mnangagwa
HARARE
Aliyekuwa makamu wa rais wa Zimbabwe Emmerson
Mnangagwa ambaye amefutwa kazi wiki tatu zilizopita na kutoroka nchi hiyo
kufuatia vitisho vya kifo , anatazamia kurejea nchini leo Jumatano mchana, siku
moja baada ya rais Robert Mugabe kujiuzulu, na kuongoza Zimbabwe kwa muda
kuelekea Uchaguzi Mkuu mwaka ujao.
Emmerson Mnangagwa anatazamia kuchukua hatamu ya
uongozi wa nchi baada ya kuteuliwa katika mkutano wa hadhara wa chama cha
Zanu-PF siku ya Jumapili kuongoza chama hicho tawala.
Kulingana na katiba ya nchi ya Zimbabwe rais
anapojiuzulu makamu wake ndio anachukua nafasi yake hadi uchaguzi mpya.
Bw. Mnangagwa atatawazwa kesho Alhamisi na hivyo
kuanza rasmi majukumu ya uongozi wa taifa la Zimbabwe, baada ya miaka 37 ya
uongozi wa Robert Mugabe.
Maelfu ya raia wa Zimbabwe walimiminika katika mitaa
ya miji mbalimbali baada ya tangazo la kujiuzulu kwa rais Robert Mugabe.
SOURCES:RFI SWAHILI.
No comments:
Post a Comment