Rais wa Urusi Vladimir Putin |
MOSCOW.
Mkutano kuhusu mchakato wa amani nchini Syria unatazamiwa
kufanyika Sochi, nchini Urusi, leo Jumatano.
Mkutano huu ni kati ya wadhamini watatu wa mchakato wa
Astana: Urusi,Uturuki na Iran.
Rais wa Urusi Vladimir Putin anataka kushawishi
wenzake wawili, Recep Tayyip Erdogan na Hassan Rohani kusaidia jitihada za
kutafuta ufumbuzi wa kisiasa kwa mgogoro wa Syria Na kuandaa mkutano nchini
Urusi kati ya upinzani wa utawala wa Bashar al Assad na serikali.
Hili ni lengo kubwa la kidiplomasia la Vladimir Putin
kukutana katika mji wa Sochi na wawakilishi wa upinzani na serikali ya Syria.
Mkutano huo utakuwa na lengo la kuunda katiba mpya ya
Syria na kutafuta ufumbuzi wa kisiasa kwa mgogoro nchini humo tangu mwaka 2011.
SOURCES:RFI SWAHILI.
No comments:
Post a Comment