MPANDA
Uhaba wa vyumba vya
madarasa katika shule za sekondari ndio chanzo kinachochangia wanafunzi
kulazimika kupangiwa shule zilizopo mbali na maeneo yao.
Hayo yamesemwa na Afisa
elimu wa Halmashauri ya Manispaa ya Mpanda mkoa Katavi Bi Helia Lukunguru
wakati akizungumza na Mpanda Redio amesema shule za sekondari zilizopo
hazitoshi kukidhi mahitaji yaliyopo kwa sasa.
Aidha ameeleza kuwa
inawalazimu kuwapangia wanafunzi shule za mbali na maeneo yao kwa sababu shule
za sekondari katika maeneo husika kushindwa kumudu idadi ya wanafunzi
wanaofaulu.
Kauli hii inakuja siku
chache baada ya wananchi kulalamika kuingia gharama zaidi.
CHANZO: REBEKA KIJA.
No comments:
Post a Comment