Sunday, 19 November 2017

ZANU PF yamvua uongozi Mugabe.




Chama cha ZANU PF cha Zimbabwe kimemvua uongozi wa chama hicho, Rais Robert Mugabe na kumchagua aliyekuwa Makamu wa Rais, Emmerson Mnangagwa kukiongoza.
Rais Mugabe alimuondoa madarakani Mnangawa wiki mbili zilizopita hivyo kuibua matukio kadhaa, likiwemo la jeshi kutwaa madaraka na kumzuia Mugabe (93), kumteua mkewe Grace kuwa makamu wa rais.
Wazimbabwe jana Jumamosi Novemba 18,2017 walishiriki maandamano kupinga utawala wa Rais Mugabe ambaye amekuwa madarakani kwa zaidi ya miaka 30 sasa.
Rais Mugabe anatarajiwa kukutana na viongozi wa jeshi la nchi hiyo na tayari msafara wa magari umeonekana ukitoka nyumbani kwake.
Kiongozi wa chama cha maveterani wa vita ya ukombozi wa Taifa hilo, Chris Mutsvangwa ameliambia Shirika la Habari la Reuters kwamba, chama hicho pia kimeanza mchakato wa kumwondoa Mugabe kama Rais wa nchi hiyo.
Reuters imeripoti kwamba Grace, mkewe Mugabe amefukuzwa uanachama.
Watu wameonekana mitaani wakicheza na kushangilia baada ya ZANU PF kumwondoa katika uongozi Mugabe.

No comments:

Featured post

MASIKINI WEEE!!!!! KICHANGA CHA SIKU MOJA CHAOKOTWA KATIKA KIWANJA CHA MPIRA AZIMIO

Na;Ezelina Yuda Mtoto mchanga mwenye jinsia ya Kike anayekadiriwa kuwa wa siku 1 ameokotwa akiwa hai kandokando ya uwanja wa azimio  ...