Monday, 4 December 2017

Mkuu wa wilaya ya Tanganyika Salehe Muhando amesema wilaya yake inachukua njia za haraka za kudhibiti kuenea kwa ugonjwa wa kipindupindu

Mkuu wa wilaya ya Tanganyika Salehe Muhando



TANGANYIKA

Mkuu wa wilaya ya Tanganyika Salehe Muhando amesema wilaya yake inachukua njia za haraka za kudhibiti kuenea kwa ugonjwa wa kipindupindu

Muhando ametoa kauli hiyo baada ya kuripotiwa visa kadhaa vyua ugonjwa huo katika maeneo mbalimbali ya wilaya ya Tanganyika

Muhando amewataka wakazi wa wilaya hiyo kufuata kanuni zote za afya za kujikinga ugonjwa huo ikiwemo kunawa mikono kwa sabuni kuchemsha maji ya kunywa na kuohsa matunda na mboga mboga kwa maji safi.

Katika hatua nyingine Muhando ameatahadharisha wakazi wote wa wilaya hiyo kuchukua hatua za madhubuti pale waonapo dalili za kipindupindu ili kuwahi kutibiwa na kuepukana imani za kishirikina kwani ugonjwa huo hauhusiani kwa namna yoyote na ushirikina


Source:Alinanuswe

No comments:

Featured post

MASIKINI WEEE!!!!! KICHANGA CHA SIKU MOJA CHAOKOTWA KATIKA KIWANJA CHA MPIRA AZIMIO

Na;Ezelina Yuda Mtoto mchanga mwenye jinsia ya Kike anayekadiriwa kuwa wa siku 1 ameokotwa akiwa hai kandokando ya uwanja wa azimio  ...