Monday, 4 December 2017

Wakili ahukumiwa kwa kuchochea ubakaji.


CAIRO

Mahakama mmoja nchini Misri imemhukumu kifungo cha miaka mitatu jela Wakili maarufu nchini humo Nabih al-Wahsh kufuatia kauli yake ya kuhamasisha kubakwa wanawake wanaovaa nguo zisizositiri miili yao.

Wakili al-Wahsh ambaye alitoa kauli hiyo kwenye mahojiano na kituo kimoja cha televisheni ametiwa hatiani kwa kuchochea ubakaji na unyanyasaji wa kingono dhidi ya wanawake ambapo hata hivyo amesomewa hukumu hiyo akiwa hayuko Mahakamani.

Waendesha mashtaka wamedai kauli ya Wakili huyo inahamasisha uvunjifu wa sheria,kutishia amani na kuhatarisha maisha ya raia wa taifa hilo la Kiarabu.

Source:eatv,

No comments:

Featured post

MASIKINI WEEE!!!!! KICHANGA CHA SIKU MOJA CHAOKOTWA KATIKA KIWANJA CHA MPIRA AZIMIO

Na;Ezelina Yuda Mtoto mchanga mwenye jinsia ya Kike anayekadiriwa kuwa wa siku 1 ameokotwa akiwa hai kandokando ya uwanja wa azimio  ...