Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais TAMISEMI, Mh. Selemani Jafo
amempa wiki sita Mkandarasi wa mradi wa maji wa Kivindo Wilayani Muheza mkoani
Tanga, kuhakikisha anakamilisha mradi huo na uanze kutoa huduma.
Waziri Jafo ametoa agizo hilo wakati wa ziara yake ya kukagua
miradi ya maendeleo wilayani Muheza, ambapo alikagua miradi katika maeneo
mbalimbali ya Halmashauri hiyo ukiwemo mradi huo wa maji.
Aidha Waziri Jafo alimtaka Mkandarasi wa Mradi huo ambao
umefikia asilimia 90 ya utekelezaji wake kuwaahidi wananchi kuwa ataukamilisha
ndani ya muda wa wiki sita ambao amepewa na waziri.
SOURCE: EATV
No comments:
Post a Comment