Friday, 5 January 2018

Baadhi ya vijana katika halmashauli ya manispaa ya Mpanda mkoani Katavi wenesema uelewa mdogo kuhusu mikopo inayotolewa na serikali ni kikwazo cha maendeleo.


MPANDA

Baadhi ya vijana katika halmashauli ya manispaa ya Mpanda mkoani Katavi  wenesema uelewa mdogo kuhusu mikopo inayotolewa na serikali ni kikwazo cha maendeleo.

Wakizungumza na Mpanda redio fm kwa nyakati tofauti wamesema milolongo ya namna ya upatikanaji wa mikopo inayowekwa na maafisa maendeleo ya jamii huongeza mbinyo zaidi.

Aidha wameiomba selikari kuingilia kati na kurekebisha mifumo ili kuwe na ushirikishwaji wa moja kwa moja utako enda samaba mba na utoaji wa elimu.

Halmashauri zote nchini hutenga asilimia kumi kwa mgawanyo wa vijana asilimia tano na wanawake asilimia tano.


 Na Paul Matius

No comments:

Featured post

MASIKINI WEEE!!!!! KICHANGA CHA SIKU MOJA CHAOKOTWA KATIKA KIWANJA CHA MPIRA AZIMIO

Na;Ezelina Yuda Mtoto mchanga mwenye jinsia ya Kike anayekadiriwa kuwa wa siku 1 ameokotwa akiwa hai kandokando ya uwanja wa azimio  ...