Friday, 5 January 2018

Wateja wa benki tano zilizotangazwa kufilisika, wataambulia kiasi cha Sh1.5 milioni ya amana zao kwa mujibu wa sheria.


DAR ES SALAAM.

Wateja wa  benki tano zilizotangazwa kufilisika, wataambulia kiasi cha Sh1.5 milioni ya amana zao kwa mujibu wa sheria.

Kaimu mkurugenzi wa bodi hiyo, Richard Malisa amEhakikishia Profesa Ndulu kuwa taratibu za malipo hayo zitafanyika haraka iwezekanavyo huku kiwango cha juu kitakacholipwa kwa wateja kikiwa ni Sh1.5 milioni.

Taasisi tano zilizotangazwa kufilisiwa ni Benki ya Wanawake Convenant na Efatha.

Nyingine ni benki za wananchi; Njombe na Meru pamoja na Benki ya Wakulima Mkoa wa Kagera (KFCB) ambazo zinaungana na FBME, Twiga Bancorp na Benki ya Wananchi Mbinga zilizofilisika na kufutiwa leseni mwaka jana.

Nyingine tatu zimewekwa chini ya uangalizi ambazo ni Benki ya Ushirika Kilimanjaro, Benki ya Wanawake Tanzania (TWB) na Benki ya Wananchi Tandahimba ambazo, endapo zitashindwa kukidhi vigezo, baada ya muda, nazo zitafilisiwa.


Chanzo: Mwananchi

No comments:

Featured post

MASIKINI WEEE!!!!! KICHANGA CHA SIKU MOJA CHAOKOTWA KATIKA KIWANJA CHA MPIRA AZIMIO

Na;Ezelina Yuda Mtoto mchanga mwenye jinsia ya Kike anayekadiriwa kuwa wa siku 1 ameokotwa akiwa hai kandokando ya uwanja wa azimio  ...