Friday, 5 January 2018

Wakazi wengi wa Mtaa wa Msasani na Tambukareli Manispaa ya Mpanda Mkoani Katavi hawajahama kupisha mipaka ya hifadhi ya reli licha ya kutakiwa kuondoka kabla ya mwezi Januari mwaka huu.


MPANDA

Wakazi wengi wa Mtaa wa Msasani na Tambukareli Manispaa ya Mpanda Mkoani Katavi hawajahama kupisha mipaka ya hifadhi ya reli licha ya kutakiwa kuondoka kabla ya mwezi Januari mwaka huu.

Wakizungumza na Mpanda Radio kwa Nyakati tofauti wamesema,baadhi yao hawajaondoka katika maeneo hayo kutokana na ukosefu wa viwanja huku wakisema baadhi ya wajumbe wa serikali ya mtaa huo wamejigawia kiwanja zaidi ya kimoja

Kwa upande wake mwenyekiti wa Mtaa wa Msasani Jonard Makoli amekanusha wajumbe wa serikali kujipatia viwanja zaidi ya kimoja ambapo amesema mchakato wa majina ya wanaotakiwa kupata viwanja ilipitia katika vikao na mikutano ya hadhara.

Zaidi ya wakazi 280 wa mitaa ya Msasani na Tambukareli wameathiriwa na tangazo la bomoabomoa lililotolewa na mwishoni mwa mwaka jana na mamlaka inayohusika na reli Tanzania.


Chanzo:Issack

No comments:

Featured post

MASIKINI WEEE!!!!! KICHANGA CHA SIKU MOJA CHAOKOTWA KATIKA KIWANJA CHA MPIRA AZIMIO

Na;Ezelina Yuda Mtoto mchanga mwenye jinsia ya Kike anayekadiriwa kuwa wa siku 1 ameokotwa akiwa hai kandokando ya uwanja wa azimio  ...