Sunday, 14 January 2018

Meli ya mafuta iliyokuwa ikiteketea moto imezama baharini.



Meli ya mafuta iliyokuwa ikiteketea moto imezama bahariniHaki miliki ya picha
Image captionMeli ya mafuta iliyokuwa ikiteketea moto imezama baharini
Meli ya mafuta ambayo imekuwa ikiteketea kusini mwa bahari ya China kwa zaidi ya wiki moja hatimaye imezana, kwa mujibu wa vyombo vya habari vya China.
Sanchi na meli nyingine ya mizigo ziligongana kilomita 260 nje ya Shanghai tarehe 6 Januari ambapo baadaye ilianza kusombwa kusini mashariki kwenda Japan.
Maafisa wa Iran sasa wanasema kuwa wahudumu wote 32, wakiwemo raia 30 wa Iran na wawili raia wa Bangladesh wote walifariki.
Meli hiyo ilikuwa imebeba tani 136,000 za mafuta lakini maafisa wanasema kuwa hakuna hatari kubwa.
Meli hiyo ilikuwa imebeba tani 136,000 za mafuta lakini maafisa wanasema kuwa hakuna hatari kubwa.
Image captionMeli hiyo ilikuwa imebeba tani 136,000 za mafuta lakini maafisa wanasema kuwa hakuna hatari kubwa.
Meli zingine 13 na kikosi kutoka Iran wamekuwa wakishiriki katika jitihada za kuokoa licha ya kuwepo hali mbaya ya hewa.
Siku ya Jumamosi wafanyakazi walikuwa wameingia kwenye meli hiyo ambapo walipata miili ya wahudumu wawili ndani ya mashua ya kuokoa maisha.
Waokoaji walipata kisanduku cha kurekodi sarafi lakini wakaondoka haraka kutokana kuwepo moshi na joto jingi.
Chanzo:Bbc swahili

No comments:

Featured post

MASIKINI WEEE!!!!! KICHANGA CHA SIKU MOJA CHAOKOTWA KATIKA KIWANJA CHA MPIRA AZIMIO

Na;Ezelina Yuda Mtoto mchanga mwenye jinsia ya Kike anayekadiriwa kuwa wa siku 1 ameokotwa akiwa hai kandokando ya uwanja wa azimio  ...