Mwenyekiti wa Taifa balaza la wanawake la Chama cha Democrasia na Maendeleo Chadema Ambae ni mbunge wa jimbo la Kawe Halima Mdee |
KATAVI
Mwenyekiti wa Taifa balaza la wanawake la Chama cha Democrasia na
Maendeleo Chadema Ambae pia ni mbunge wa
jimbo la Kawe Halima Mdee amezitaka taasisi za ndani ya chama hicho kuwajibika
vyema katika kukijenga chama hicho.
Akizungumza na wanawake wa chama hicho pamoja na vijana katika shule ya sekondari ya Mtakatifu Maria manispaa ya Mpanda amesema Taasisi hizo kwa kushilikiana na vijana vinamchango mkubwa katika kukijenga chama hicho Hapa nchini
Kwa upande wake mbunge wa viti maalumu wa chama hicho katika Mkoa wa Katavi Rhoda Kunchela amesema kunavikundi mbalimbali vya akina ambavyo vimeanza kunufaika.
Ziara hiyo ya mwenyekiti wa Bawacha Taifa
inalengo la kukagua uhai wa jumuia hiyo
na chama kwa ujumla katika mikoa ya Rukwa Tabora na Katavi
ugeni huo umeambatana na katibu mkuu wa balaza la wanawake la chama
hicho Taifa Grace Tendega.
Chanzo: Paul Martius
No comments:
Post a Comment