RAIS wa Zanzibar Dkt. Ali Mohamed Shein |
ZANZIBAR
RAIS wa Zanzibar Dkt.Ali Mohamed Shein
ametangaza kuwa kuanzia mwezi Julai mwaka huu, michango yote iliyokuwa ikitolewa
na wazazi katika elimu ya sekondari visiwani Zanzibar itafutwa.
Rais Shein ametanagaza hatua hiyo jana katika
maadhimisho ya miaka 54 ya Mapinduzi ya Zanzibar yanayoadhimishwa Januari 12 ya
kila mwaka.
Amesema hatua hiyo inachukuliwa kutokana na
kuimarika kwa uchumi na ukusanyaji wa mapato ambapo Serikali ya Mapinduzi ya
Zanzibar inakusudia kuimarisha huduma za afya na elimu.
Dk.Shein amesema uamuzi huo unakwenda sambamba
na kutekeleza dhamira ya Rais wa Kwanza wa Zanzibar,Abeid Amani Karume
aliyetangaza elimu bure kwa wananchi wote.
Rais Shein akielezea hali ya ukusanyaji wa
mapato,amesema Zanzibar imepiga hatua kubwa kupitia taasisi zake za kodi
Zanzibar (ZRB) na Tanzania (TRA) ambapo jumla ya Sh bilioni 548.57 zilikusanywa
katika mwaka 2017 ukilinganishwa na Sh bilioni 487.474 zilizokusanywa katika
mwaka 2016.
Chanzo:Habari
leo
No comments:
Post a Comment