Mwenyekiti wa TLP Mh. Augustine Mrema |
DAR ES SALAAM
Sakata la kuzushiwa kifo Mwenyekiti wa
TLP,Augustine Mrema limechukua sura mpya baada ya kiongozi huyo kutaka
waliosambaza taarifa hizo wamlipe fidia ya Shilingi bilioni ishirini kutokana na usumbufu
alioupata.
Mrema ambaye pia ni Mwenyekiti wa Bodi ya Parole
amesema hayo jana mara baada ya kufika Kituo cha Polisi Osterbay kutoa taarifa
za uzushi huo aliodai umemsababishia usumbufu yeye, ndugu zake na watoto wake.
Januari 9,katika mitandao mbalimbali ya kijamii zilisambaa
taarifa za kufariki dunia kwa mwanasiasa huyo mkongwe nchini katika Hospitali
ya KCMC- Moshi mkoani Kilimanjaro.
Amesema lengo la kusambaza ujumbe huo ilikuwa ni
mikakati ya wanasiasa kuharibu utendaji wake wa kazi ikiwamo kuvuruga mkutano
wa hadhara aliokuwa amepanga kuufanya siku hiyo.
Kwa upande wa Kamanda wa Polisi Mkoa wa
Kinondoni, Jumanne Murilo amesema suala hilo la Mrema linalishughulikiwa kwa
taratibu za jeshi hilo na watakaobainika watachukuliwa hatua.
Chanzo: Mwananchi
No comments:
Post a Comment