Saturday, 13 January 2018

Maandamano makubwa yameendelea kufanyika nchini Tunisia na kusababisha vurugu za kimabavu.

Waandamanaji wa Tunisia


TUNIS

Maandamano makubwa yameendelea kufanyika nchini Tunisia na kusababisha vurugu za kimabavu.

Wizara ya mambo ya ndani ya Tunisia imesema, vurugu hizo zilizotokea jana zimesababisha kifo cha raia mmoja na askari zaidi 60 kujeruhiwa huku magari zaidi 50 yakiharibiwa na watu wasiopungua 600 wamekamatwa.

Msemaji wa wizara ya mambo ya ndani Khalifa Al-Shaibani amesema kuna vijana wengi miongoni mwa waandamanaji waliokamatwa wanaohusishwa na vitendo vya uporaji,wizi na uchomaji moto ambavyo vimevuruga utaratibu wa jamii.

Maandamano hayo yanadiawa kutokana na kuongezeka kwa gharama za maisha na sheria ya fedha ya mwaka 2018 ambayo imesababisha kuongezeka kwa bei ya bidhaa.


Chanzo:CRI

No comments:

Featured post

MASIKINI WEEE!!!!! KICHANGA CHA SIKU MOJA CHAOKOTWA KATIKA KIWANJA CHA MPIRA AZIMIO

Na;Ezelina Yuda Mtoto mchanga mwenye jinsia ya Kike anayekadiriwa kuwa wa siku 1 ameokotwa akiwa hai kandokando ya uwanja wa azimio  ...