Rais wa Marekani Donald Trump |
WASHINGTON DC
Nchi 54 za Afrika zimemtaka Rais wa Marekani
Donald Trump kuziomba radhi baada ya kuripotiwa kutumia maneno machafu
alipokuwa akizungumzia kuhusu wahamiaji kutoka mataifa ya Afrika,Haiti na El
Salvador wakati alipokutana na wabunge kwenye Ikulu.
Baada ya kikao cha dharura cha mabalozi wa nchi
za Afrika ambacho kimefanyika nchini Marekani,mabalozi hao wamesema wanatiwa
wasiwasi na mtindo unaozidi kujitokeza kwenye utawala wa Marekani na wamelaani
vikali matamshi ya kibaguzi ya kudumisha chuki dhidi ya wageni.
Chanzo cha mvutano huo ni baada ya Trump kuuliza
kuwa kwa nini Marekani iwapokee wahamiaji kutoka nchi za uozo kama za Afrika,Haiti
na El Salvador.
Hata
hivyo Rais Donald Trump amekanusha kutumia maneno machafu juu ya nchi kadhaa
ikiwa pamoja na nchi za Afrika.
Chanzo: CRI
No comments:
Post a Comment