Naibu waziri wa Wizara ya Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto Dk.Faustine Ndugulile |
KATAVI.
Naibu waziri wa Wizara ya Afya,Maendeleo
ya Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto Dk.Faustine Ndugulile amewataka watanzania
kuhakikisha watoto wote wanapatiwa haki zote za msingi katika maisha yao
ikiwemo haki za kuishi na kulindwa.
Dkt.Ndugulile ametoa wito huo Mjini
Mpanda wakati akizungumza na Makundi mbalimbali ya wananchi ambayo yamepewa
jukumu la kuelimisha jamii kuhusu haki za mtoto na kuwaibua watoto wanaoishi
katika mazingira hatarishi.
Aidha DK.Ndugulile amesema serikali
itaendelea kushirikiana na Shirika la JSI la Marekani linalojihusisha na masuala
ya jamii ikiwemo kudhibiti mambo yanayomkatisha mtoto kutimiza ndoto zake hasa
kielimu.
Kwa upande wake Afisa Ustawi wa Jamii
Manispaa ya Mpanda Bi.Redgunda Mayorwa amesema ushirikiano kati ya serikali na
wadau mbalimbali ndiyo njia pekee itakayomukoa mtoto dhidi ya mazngira
hatarishi ikiwa ni pamoja na wanaishi na maambukizi ya virusi vya Ukimwi.
Flora Cosmas kutoka Manispaa ya
Mpanda ambaye ni Miongoni mwa watoa huduma ngazi ya jamii katika masuala ya
mbalimbali ikiwemo ukatiri wa kijinsia pamoja na mambo mengine amesema
Halmashauri ya Manispaa ya Mpanda ina jumla ya wasimamizi wa mashauri ya watoto
ngazi ya jamii wapatao 90 wakiwemo wanaume 40 na wanawake 50 huku wasimamizi
viongozi wakiwa 15 wanaume 8 na wanawake 7.
Aidha amesema jumla ya watoto 1200 na
wazazi walezi 506 waishio katika mazingira wameibuliwa na kupatiwa huduma
katika maeneo mablimbali ya Manispaa ya Mpanda.
Katika Mkoa wa Katavi kumekuwa
kukiripotiwa kesi kadhaa za watoto kunyanyaswa,kutupwa katika mazingira
hatarishi mara baada ya kuzaliwa na
kutopatiwa haki za msingi ikiwemo elimu ambao nguvu ya jamii inatakiwa kutumika
ipasavyo ili kukomesha matukio hayo ili kumlinda mtoto.
Chanzo: Issack Gerald
No comments:
Post a Comment