Friday, 12 January 2018

Trump akataa kufungua ubalozi mpya wa Marekani Uingereza.



Waziri mkuu wa Uingereza bi Theresa May na mwenzake wa Marekani Donald Trump alipozuru taifa hilo.Haki miliki ya picha
Image captionWaziri mkuu wa Uingereza bi Theresa May na mwenzake wa Marekani Donald Trump alipozuru taifa hilo.
Rais Donald Trump wa Marekani amefutilia mbali mpango wa kuzuru nchini Uingereza mnamo mwezi Februari ambapo alikuwa ametarajiwa kufungua ubalozi mpya wa taifa hilo uliogharimu takriban dola bilioni moja.
Katika ujumbe wake kwa Twitter, rais huyo wa Marekani alisema yeye sio shabiki wa ubalozi huo mpya ambao unahamia kutoka Mayfair kuelekea mjini London akidai kuwa ulikuwa ''mpango mbaya''.
''Jumba la zamani la ubalozi huo liliuzwa kwa fedha chache na utawala wa rais Obama'', aliongezea.
Downing Street ilikataa kutoa tamko kuhusu hatua hiyo ya rais Trump.
Muhariri wa BBC kaskazini mwa Marekani Jon Sopel alisema kuwa kuna uwezekano wa maandamano katika barabara za mji wa London iwapo angezuru.
Hatua hiyo ya ubalozi wa Marekani ilithibitishwa mnamo mwezi Oktoba 2008 wakati rais George W Bush alipokuwa mamlakani.
Ujumbe wa rais Trump aliouweka katika mtandao wa twitterHaki miliki ya pichaTWITTER
Image captionUjumbe wa rais Trump aliouweka katika mtandao wa twitter
Hata hivyo Rais Trump aliulaumu utawala wa aliyekuwa rais wa taifa hilo Barrack Obama kwa kuuza eneo zuri la ubalozi huo kwa ''fedha chache''.
Alisema kuwa jengo hilo jipya katika eneo la Vauxhall, kusini mwa London lilikuwa katika eneo baya, akiongezea.''Walitaka mimi nilifungue rasmi-Hapana!''
Chanzo:Bbc swahili

No comments:

Featured post

MASIKINI WEEE!!!!! KICHANGA CHA SIKU MOJA CHAOKOTWA KATIKA KIWANJA CHA MPIRA AZIMIO

Na;Ezelina Yuda Mtoto mchanga mwenye jinsia ya Kike anayekadiriwa kuwa wa siku 1 ameokotwa akiwa hai kandokando ya uwanja wa azimio  ...