Friday, 12 January 2018

Rais wa Zanzibar, Dk Ali Mohammed Shein amewataka wananchi wa Zanzibar kuendelea kudumisha amani na utulivu .








ZANZIBAR

 Rais wa Zanzibar, Dk Ali Mohammed Shein amewataka wananchi wa Zanzibar kuendelea kudumisha amani na utulivu uliopo ili kuwa chachu ya kuendelea kuwa kivutio kikubwa kwa uwekezaji miradi mikubwa ya maendeleo visiwani humo.

Amesema hayo Katika maadhimisho  ya miaka 54 ya Mapinduzi ya Zanzibar yaliyo udhuriwa na Rais wa Tanzania Dk John Pombe Magufuli na viongozi wengine wa serikali ambapo  ameelezea kukua kwa kasi ya uchumi katika visiwa hivyo na kuwa lengo la kuimarisha uchumi ni endelevu.

Ameutaja mradi wa kusaidia kaya masikini  Tasaf namba tatu  kuzinufaisha kaya zaidi ya 32478 ikiwa nikiwango kikubwa zaidi.

Aidha amesema serikali ya mapinduzi ya Zanzibar itaendelea kuwainua wakulima kwa kusimamia misingi ya kisera akilitaja zao la kalafuu Kama zao lenye tija zaidi.

Zanzimbar iliungana na Tanganyika mnamo apr 26, 1964 chini ya  waasisi hayati Sheihk Abeid Aman Karume na hayati Mwalimu Julius Kambarage Nyerere.


Chanzo: TBC

No comments:

Featured post

MASIKINI WEEE!!!!! KICHANGA CHA SIKU MOJA CHAOKOTWA KATIKA KIWANJA CHA MPIRA AZIMIO

Na;Ezelina Yuda Mtoto mchanga mwenye jinsia ya Kike anayekadiriwa kuwa wa siku 1 ameokotwa akiwa hai kandokando ya uwanja wa azimio  ...