MPANDA
Baadhi ya wakulima
katika kata ya Magamba kitongoji cha Makongoro Mkoa wa Katavi wameiomba
serikali kusaidia kupata pembejeo za kilimo kwa wakati ili kuongeza uzalishaji
wa mazao.
Wakizungumza na Mpanda
redio kwa nyakati tofauti wakazi hao wamesema kwamba ucheleweshwaji wa pembejeo katika kitongoji hicho kimewaathiri
hali iliyopelekea kushindwa kuzalisha mazao ya biashara kwa wingi.
Aidha wamesema kwa sasa
wengi wao wanatumia mbolea ya ng’ombe ambayo napatikana kwa uchache hivyo
kusababisha mazao kuharibika.
Wananchi wameiomba
serikali kuwasaidia kupata pembejeo za kilimo kwa wakati na kwa bei nafuu
zitakazosaidia kufanya shughuli zao za kilimo kwa uhakika zaidi.
Chanzo: Alinanuswe
No comments:
Post a Comment