Monday, 12 February 2018

Mkahakama kuu kanda ya Sumbawanga imeanza vikao vyake kwa kuanza kusikiliza kesi mbalimbali zikiwemo za mauaji,uhujumu uchumi,katika mahakama ya Hakim mkazi mkoani katavi.


KATAVI

Mkahakama kuu kanda ya Sumbawanga  imeanza vikao vyake  kwa kuanza  kusikiliza kesi mbalimbali zikiwemo za mauaji,uhujumu uchumi,katika mahakama ya Hakim mkazi mkoani katavi

Naibu msajili ya mahakama kanda ya sumbawanga Romuli Mark Mbuya akizungumza na mpanda redio amesema kuwa kesi hizo na mashauri hayo yatasikilizwa na jaji Dr Adam Mambi wa kanda ya sumbawanga.

Aidha NAIBU Msajili Mbuya amefafanua kuwa miongoni mwa mashauri hayo 13 mawili  yalikatiwa rufaani  kwenda mahakama ya rufani na mahakama hiyo kuamuru kuanza kusikiliza upya

Hata hivyo wananchi wametakiwa kujitokeza kusikiliza muendelezo wa vikao hivyo vya kesi hizo vitakavyodumu kwa muda wiki mbili mfululizo

Chanzo: Edward Mganga
#Changia Damu Okoa Taifa

No comments:

Featured post

MASIKINI WEEE!!!!! KICHANGA CHA SIKU MOJA CHAOKOTWA KATIKA KIWANJA CHA MPIRA AZIMIO

Na;Ezelina Yuda Mtoto mchanga mwenye jinsia ya Kike anayekadiriwa kuwa wa siku 1 ameokotwa akiwa hai kandokando ya uwanja wa azimio  ...