Monday, 12 February 2018

Madereva bodaboda wameliomba jeshi la polisi kitengo cha usalama barabarani kutekeleza sheria bila uonevu.



MPANDA

Siku chache baada ya kuadhimisha wiki ya nenda kwa usalama barabarani baadhi ya madereva bodaboda wameliomba jeshi la polisi kitengo cha usalama barabarani kutekeleza sheria bila uonevu.

Wakizungumza kwa nyakati tofauti wameeleza kuwa utendaji wa haki katika majukumu ya kipolisi utachangia kupunguza ajari zisizo za lazima.

Katika hatua nyingine wamesema kuwa vitendo vya rushwa kwa kiasi kikubwa vimetokana na uelewa mdogo miongoni mwao kuhusu utambuzi wa makosa ya usalama barabarani ikiwemo na woga dhidi ya Jeshi la polisi.

Wiki ya Usalama barabarani mkoani Katavi imefikia kilele ijumaa iliyopita ikiwa na kauli mbiu ya Tii sheria okoa maisha kata rushwa.


Chanzo: Haruna Juma
#Changia Damu Okoa Taifa

No comments:

Featured post

MASIKINI WEEE!!!!! KICHANGA CHA SIKU MOJA CHAOKOTWA KATIKA KIWANJA CHA MPIRA AZIMIO

Na;Ezelina Yuda Mtoto mchanga mwenye jinsia ya Kike anayekadiriwa kuwa wa siku 1 ameokotwa akiwa hai kandokando ya uwanja wa azimio  ...