TANGANYIKA
Baraza la Madiwani katika Halimshauri ya wilaya ya Mpanda wilaya ya Tanganyika Mkoa wa Katavi limeidhinisha jumla ya miradi sita ya maendeleo itakayo tekelezwa na Fedha za Mradi kutoka Ruzuku ya mtaji LGDG kwa mwaka 2017/2018
Akiwasilisha
hoja hiyo mbele ya kikao maalumu cha baraza la madiwani kilichofanyika katika
ukumbi wa mikutano wa idara ya maji kaimu afisa mipango wa halimashauri ya
wilaya ya Mpanda bwana Philimoni Mlageli ameitaja baadhi ya miradi itakayo
tekelezwa katika Mpango huo kuwa ni pamoja na ujenzi wa stendi katika kijiji
cha ikola pamoja na miradi mingine
Kwa
upande wake diwani wa kata ya Kalema Maiko Kapata amesema ametumia nafasi hiyo
kuliomba Baraza kubadilisha matuminzi ya pesa yaliyotengwa kwa jaili ya
ukarabati wa shule ya msingi kalema na badala yake pesa hiyo ielekezwe katika
utekelezaji wa mradi wa maji katika kijiji cha itetemia
Naye
kaimu afsa mipango Bwana Filemon Mlageli amebainisha kuwa mashart ya pesa hizo
ni mpaka miradi ikamilike
Miradi
hiyo kwa pamoja inatarajia kughalimu zaidi ya shilingi billion moja za
kitanzani hadi kukamilika kwake.
Chanzo: Poul Mathias
No comments:
Post a Comment