TANGANYIKA
Wakulima wa mazao ya pamba na korosho
katika kijiji cha Nkungwi kata ya Sibwesa wilaya ya Tanganyika Mkoani
Katavi wameiomba serikali kuendelea
kutoa elimu juu ya matumizi ya pembejeo hususani dawa za kuulia wadudu.
Hayo yamesemwa na baaadhi ya wakulima
katika ziara ya Mkuu wa Mkoa Meja Jenerali Mstaafu Raphaeli Muhuga ya ukaguzi
wa mazao mapya mkoani hapa na kusema kuwa mazao yamekuwa yakiharibiwa na
wadudu hususani zao la pamba.
Kwa upande wake Mkuu wa mkoa amesema kuwa
maafisa ugani wanapaswa kushirikiana katika kutatua tatizo hilo kwani baadhi ya
maeneo hayana tatizo la wadudu huku wakulima hao wakitumia aina moja ya dawa.
Kutokana na halimashauri zote Mkoani
katavi kutegemea zao la Tumbaku na zao hilo kushuka soko kumepelekea kuanzishwa kwa mazao mapya
ya biashara ikiwemo korosho,pamba na alizeti mazao ambayo yamepewa kipaumbele
kitaifa ili kuweza kusaidia wakulima kujikwamua kiuchumi.
Chanzo:Restuta Nyondo
No comments:
Post a Comment