MPANDA.
Vijana wanne wanao sadikiwa kuwa ni
vibaka wamevunja na kuiba mchele kilo 240 wenye thamani ya shilingi laki tatu
katika eneo la viwanda vya kukoboa mchele la mpanda hotel katika halimashauri
ya manispaa ya Mpanda mkoa wa katavi.
Akizungumza na mpanda redio Meneja wa
kiwanda hicho Emmanuel Samadali amesema wizi huo umetokea usiku wa kuamkia leo
katika eneo hilo na baada hatua hiyo walianza kufuatilia tukio hilo kwa baadhi
ya vijana ambao walionekana kuranda randa pasipo kuwa na shughuli ya kufanya
katika eneo hilo.
Bwana samadali amesema baada ya kufanya
upekuzi kwa vijana hao wamekuta kiasi hicho cha mchele vikiwa vimefungwa katika
viroba vya mifuko na hatua za kuwapeleka kituo cha polisi zinaendelea kwa ajili ya mahojiano zaidi kuhusu wizi huo.
Kwa upande wake mlinzi wa kiwanda hicho
Cypirian Antony amesema vibaka hao wamepitia upenyo wa kiwanda hicho upande wa
nyuma na kufanya wizi huo pasipo yeye kufahamu.
Chanzo:Paul Mathias
No comments:
Post a Comment