Mkuu wa Mkoa wa Manyara, Alexander Mnyeti
MANYARA
Mkuu wa Mkoa wa Manyara,
Alexander Mnyeti amelivunja baraza la ardhi la Kata ya Murray wilayani Mbulu
mkoani Manyara baada ya wananchi kulalamika kunyanyaswa, kuombwa rushwa
na kunyimwa haki zao.
Baada ya kulivunja baraza hilo,
Mnyeti amesema hawezi kuliacha liendelee kufanya kazi kwenye eneo hilo wakati
wananchi wanalalamikia kukosa haki zao.
Amemuagiza Mkurugenzi wa
Halmashauri ya mji wa Mbulu, Anna Mbogo kuanza mchakato wa kupatikana viongozi
wapya, waadilifu wa baraza la kata hiyo ili waendelee kuwatumikia wananchi.
Pia, Mnyeti amemuagiza mkuu wa
polisi wilaya ya Mbulu, kumkamata Mwenyekiti wa kijiji cha Murray, John Amme
kwa kuwanyanyasa wananchi yakiwamo madai ya kuwapiga.
Chanzo:Mwananchi
#Changia Damu Okoa Taifa
No comments:
Post a Comment