Dodoma.
Serikali imewezesha kukamilishwa utiaji saini mkataba wa ununuzi wa tumbaku
kati ya kampuni ya Premium Active Tanzania Ltd na Chama Kikuu cha Ushirika
wilaya za Songea na Namtumbo (Sonamcu Ltd).
Naibu
Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Stella Manyanya amesema mkataba huo
wa miaka saba umeanza katika msimu wa 2018/19 hadi 2025/26.
Ametoa
kauli hiyo bungeni leo mjini Dodoma alipojibu swali la mbunge wa Viti Maalumu
(CCM), Jacqueline Msongozi aliyetaka kujua Serikali ina mpango gani wa kufufua
kiwanda cha Sonamcu kilichopo Songea.
Naibu
waziri amesema mwezi huu wa Februari Serikali itapeleka Songea wahandisi wawili
kutoka nchi ya Italia watakaoshirikiana na waliopo kuandaa gharama halisi za
ukarabati wa mtambo.
Amesema tumbaku yote itakayozalishwa msimu wa 2018/19 itasindikwa katika kiwanda cha Songea.
Chanzo:Mwananchi
#Changia Damu Okoa Taifa
No comments:
Post a Comment