MPANDA
Wazee wilayani Mpanda mkoa wa Katavi
wameipongeza serikali kwa kuimarisha huduma ya afya ikiwemo mpango wa matibabu
bure kwa wazee.
Katika mazungumzo na
Mpanda radio fm wameelezea namna wanavyo pewa kipaumbele tofauti na hapo awali
ambapo iliwalazimu kubakia kwenye foleni wakisubiri matibabu.
Dokta Jafari Kitambwa Mgaganga mkuu wa Hospitali ya
Manispaa ya Mpanda amesema kuwa huduma zote zinatolewa bure kuanzia upimaji,
matibabu na Upasuaji.
Pia amesema kuwa
serikali imetenga wahudumu maalumu ambao wanahusika na utoaji huduma kwa wazee
ili kuwatenganisha na makundi mengine hospitalini kuepusha msongamano wa
wagonjwa.
No comments:
Post a Comment