Thursday, 15 February 2018

Waumini wa dini ya kikristo mkoani Katavi wametakiwa kuwa karibu na Mungu wakati wote na kuacha tabia ya kumkumbuka Mungu katika kipindi cha kwaresima pekee.



KATAVI

Waumini wa dini ya kikristo mkoani Katavi wametakiwa kuwa karibu na Mungu wakati wote na kuacha tabia ya kumkumbuka Mungu katika kipindi cha kwaresima pekee.

Hayo yamesemwa na mchungaji wa Kanisa La Kiinjili la Kilutheri Tanzania KKKT usharika wa Mpanda mjini  Shekilandi Foya wakati akizungumza na Mpanda Redio ambapo amesema waumini lazima wajenge tabia ya kumkumbuka Mungu kila mara na kuacha kusubiri kutenda mema katika kipindi cha kwaresima.

Aidha ameeleza kuwa katika kipindi hiki cha kwarezima waumini wanafunga na kutubu kwa  yale waliyo mkosea Mungu ili aweze kuwarehemu na kuwasamehe makosa .

Kwa upande wa waumini wamesema kila mkristo lazima akumbuke matese ya  Kristo kw akufunga na kutenda matendo ya liyo mema kwa wengine.

Mwezi wa Kwarezima umeanza jana kwa waumini wa kikristo ambao utahitimishwa mwezi wa Nne  tarehe moja siku ya pasaka ambayo huadhimishwa kila mwaka.

CHANZO:PAULO


No comments:

Featured post

MASIKINI WEEE!!!!! KICHANGA CHA SIKU MOJA CHAOKOTWA KATIKA KIWANJA CHA MPIRA AZIMIO

Na;Ezelina Yuda Mtoto mchanga mwenye jinsia ya Kike anayekadiriwa kuwa wa siku 1 ameokotwa akiwa hai kandokando ya uwanja wa azimio  ...